#Local News

UTABIRI WAONYESHA MVUA KUENDELEA

Wakazi walio katika nyanda za juu za eneo la kati mwa nchi, Magharibi na mwambao wa pwani wametahadharishwa kuhusu kubwa itakayoendelea katika kipindi cha kuanzia leo hadi Jumatatu wiki ijayo.

Kwenye ubashiri wake wa wiki moja, idara ya utabiri wa hali ya anga imesema manyunyu pia yanatarajiwa katika baadhi ya maeneo ya South Rift, nyanda za chini za kusini mashariki na kaskazini mashariki.

Idara hiyo imeonya kuwa huenda uchukuzi ukatatizika katika maeneo yaliyo katika hatari ya kufurika na kutaka umma ufuatilie taarifa rasmi.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *