#Local News

BODI YA SUKARI YAWAHAKIKISHIA WAKULIMA MALIPO KWA WAKATI

Bodi ya sukari nchini imewahakikishia wakulima wa miwa kuwa serikali inachukua hatua madhubuti kuhakikisha wanapokea malipo yao kwa wakati unaofaa kutoka kwa viwanda vya kusaga sukari.

Akizungumza katika jiji la Nairobi wakati wa mkutano wa sekta ya sukari barani Afrika, Afisa Mkuu wa bodi hiyo Jude Chesire amesema mageuzi ya hivi karibuni yamesaidia kurejesha imani ya wakulima.

Ameeleza kuwa serikali imeanzisha mikataba ya usambazaji iliyosanifiwa, ambayo sasa ni ya lazima kwa viwanda vyote, ili kuimarisha uwazi na uwajibikaji katika sekta hiyo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *