JUNIOR STARLETS WAINUA MATUMAINI YA KOMBE LA DUNIA
Kikosi cha timu ya taifa ya wanawake ya soka kwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17, Junior Starlets, kiliimarisha matumaini yao ya kufuzu dimba la kombe la dunia kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Namibia katika mkondo wa kwanza wa mechi za kufuzu mashindano ya FIFA U17 Women World Cup.
Wakiwa ugenini, chipukizi hao walionyesha ukomavu na utulivu, na kuchukua uongozi wa mabao 2 katika dakika za ufunguzi.
Lindey Weey alifunga bao la kwanza katika dakika ya 3, kabla ya Faith Boke kuongeza la pili.
Hata hivyo, Namibia walifuta machozi katika pambano lililoweka wazi uwezo na udhaifu wa kikosi cha Kenya kuelekea mkondo wa pili.
Kikosi hicho kinachonolewa na Mildred Cheche kitaialika Namibia kwa mechi ya marudiano Jumamosi ijayo kikilenga kudhibiti mchezo na kusalia kileleni.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































