#Local News

ATANDI APINGA HOJA YA KUMWONDOA ORENGO

Mbunge wa Alego Usonga, Samuel Atandi, amepinga wito unaoendelea wa kumwondoa madarakani Gavana wa Siaya, James Orengo, akisema hatua hiyo si ya lazima wakati uchaguzi mkuu ujao ukiwa umesalia muda mfupi.

Atandi amesema hatashiriki mjadala wa kumwondoa Orengo, akisisitiza kuwa badala yake gavana huyo anapaswa kupingwa kupitia kura katika uchaguzi.

Mbunge huyo ameeleza kuwa hakuna haja ya kumng’oa gavana huyo madarakani, akionya kuwa mchakato huo utakuwa kupoteza muda na rasilimali, na unaweza kuwazuia viongozi kuzingatia masuala ya maendeleo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *