#Football #Sports

NEKESA AAPA USHINDI KABLA YA MECHI DHIDI YA AUSTRALIA

Mshambuliaji wa Harambee Starlets, Valerie Nekesa, amesema haogopi mechi ya fainali dhidi ya Australia katika michuano ya Fifa Global Series itakayofanyika kwenye Uwanja wa Nyayo.

Nekesa amesema nafasi za viwango vya ubora duniani hazitakuwa na maana wakati timu hizo zitakapoingia uwanjani, akisisitiza kuwa kila timu itakuwa na nafasi sawa ya ushindi.

Mechi hiyo inatazamwa kuwa mtihani mkubwa kwa Harambee Starlets, huku Australia wakitajwa kuwa na nafasi kubwa ya kushinda kutokana na uzoefu na ubora wao.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *