#Local News

SAKAJA AONGOZA UBOMOAJI WA UKUTA WA IKULU KUREJESHA MTO NAIROBI

Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja anaongoza mpango wa kubomoa sehemu ya ukuta wa Ikulu ya Nairobi ulioko kwenye mkondo wa mto, katika jitihada za kurejesha Mto Nairobi.

Kulingana na Sakaja, sehemu ya ukuta huo iliyojengwa kwenye ukingo wa Kirichwa River pamoja na majengo yote yaliyo kwenye mkondo wa mto yataondolewa.

Ameeleza kuwa hatua hiyo ni ishara ya uongozi thabiti, akibainisha kuwa Rais ameonyesha mfano kwa kukubali kufuata kanuni za mazingira.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *