#Local News

RAIS AIDHINISHA BAJETI YA ZIADA

Rais William Ruto ameidhinisha mswada wa matumizi ya ziada wa mwaka 2026, hatua inayoruhusu ongezeko la matumizi ya serikali ya shilingi bilioni mia tatu sitini na tatu, zaidi ya pendekezo la awali la hazina.

Hafla ya utiaji saini ilifanyika katika Ikulu, huku kukiwa na wasiwasi unaoongezeka kuhusu deni la taifa na usimamizi wa fedha za umma.

Hatua hiyo itasababisha bajeti ya mwaka 2026/2027 kuongezeka hadi shilingi trilioni nne nukta sita, jambo linalozua mijadala miongoni mwa wataalamu wa uchumi na wananchi kuhusu matumizi na ukopaji endelevu.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

RAIS AIDHINISHA BAJETI YA ZIADA

TUJU AACHILIWA KWA DHAMANA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *