#Business

KENYA YAWEKA JUHUDI ZA BIASHARA PASI USHURU NA INDIA

Kenya inalenga kuweka mkataba wa India utakaowezesha uuzaji na uagizaji wa bidhaa baina ya mataifa hayo bila kutozwa ushuru, FTA.

Mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi, amesema Nairobi iko tayarisha kutanua uhusiano wake wa kibiashara na New Delhi kupitia mfumo mwafaka.

Lengo la Kenya na kuongeza soko la bidhaa zake na vile vile kuangazia ukosefu wa usawa katika makubaliano ya kibiashara kati yake na India.

Kulingana na takwimu, mauzo ya Kenya nchini humo ni shilingi bilioni 19.9, ikilinganishwa na bidhaa za shilingi bilioni 275.1 ambazo India huuza humu nchini, zikiweka wazi pengo lililopo.

Bidhaa kuu ambazo India huuzia Kenya ni vifaa vya matibabu, mashine, bidhaa za nguo na bidhaa za petroli iliyo tayari kutumika huku Kenya ikiuza majani chai, kahawa na maua.

Mpango wa FTA uliopendekezwa ni sehemu ya mkakati mpana wa Kenya kupanua uhusiano wa kibiashara na washirika wa kimataifa na kuongeza masoko ya bidhaa zake.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *