SEKTA YA MAJANI CHAI YAONYESHA UKUAJI – KENYA
Sekta ya majani chai nchini imeonyesha ukuaji kwa kiasi kikubwa, ikiandikisha thamani ya Shilingi bilioni 218.79 sokoni katika bajeti ya mwaka uliopita.
Hata hivyo, Ukuaji huo umehusishwa na mikakati thabiti ya mauzo na mageuzi yanayoungwa mkono na serikali ambayo yamepanua soko la Kenya kimataifa kutoka masoko 96 hadi 100 ya kuuza mazao ng’ambo.
Kufuatia ripoti ya Utendakazi wa Sekta ya majanichai iliyotolewa hivi karibuni na Bodi ya Majanichai nchini (TBK), mapato ya sekta hiyo yaliongezeka hadi kufikia Sh186.91 bilioni 2025, kutoka Sh181.69 bilioni 2024, nyongeza ya asilimia 2.87 inayowakilisha Sh5.22 bilioni kwenye mapato ya ziada.
Imetayarishwa na Maurine Amwayi
English 






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































