#Football #Sports

ZICO AREJEA POSTA RANGERS

Kocha mkongwe Zedekiah Otieno ametambulishwa rasmi kama kocha mkuu wa Posta Rangers katika uwanja wa Chuo cha Ualimu cha Thogoto.

Otieno, anayejulikana kama “Zico,” amejiunga na timu hiyo katika kipindi ambacho imekuwa ikipambana na ukosefu wa uthabiti licha ya kuanza vyema msimu.

Kwa uzoefu wa zaidi ya miaka ishirini, akiwa amewahi kuzifundisha timu kadhaa ikiwemo Gor Mahia na KCB, Zico anatarajiwa kuisaidia Posta Rangers kuboresha matokeo yake katika ligi kuu msimu unapoelekea kutamatika.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *