AFC LEOPARDS WATOA KUCHA HUKU K’OGALO WAKISUA UBINGWA
AFC Leopards wameimarisha nafasi yao katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Sportpesa kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Murang’a Seal katika Uwanja wa Nyayo Jumapili, wakikaribia kufikia viongozi na wapinzani wao wakali, Gor Mahia.
Mchezo ulianza kwa tahadhari kubwa na wasiwasi chini ya jua la Nairobi, lakini baada ya mapumziko, Ingwe walipata midhihirisho ya kiwango chao, walipata mpangilio, lengo, na ufanisi uliowawezesha kufikia pointi 55, mbili tu nyuma ya K’Ogalo.
Katika mchezo mwingine Gor Mahia walikosa kupanua pengo juu ya jedwali baada ya sare ya 0-0 katika mchezo uliochezwa uwanjani Kasarani. Kogalo walikua na nafasi nyingi lakini kutomakinika mbele ya lango kuliwakosesha alama tatu muhimu huku macho sasa yakiangazwa kwenye mashemeji derby itakayofanyika aprili 26, mchezo unaoonekana kuamua ubingwa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































