MAEGESHO HARAMU NAIROBI YAPINGWA
Mkaazi mmoja wa Nairobi amepinga kile anachodai kuwa maegesho haramu yanayofanywa na maafisa wa kaunti pamoja na wajumbe wa bunge la kaunti kwenye njia za waenda kwa miguu na maeneo ya watu wenye ulemavu katika barabara za jiji.
Katika hoja zake, amesema hatua hiyo ni matumizi mabaya ya mamlaka na ukiukaji wa haki za wananchi, akiongeza kuwa serikali ya kaunti imeshindwa kutekeleza sheria za trafiki licha ya kuwepo kwa ushahidi wa ukiukaji huo.
Hata hivyo, serikali ya kaunti pamoja na bunge la kaunti zimesema kuwa suala hilo halina msingi wa kikatiba na zimeitaka mahakama kutoingilia kwa sasa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































