#Local News

UDA PWANI YAKATAA MPANGO WA KUTENGA MAENEO

Viongozi wa chama cha UDA kutoka ukanda wa pwani wamepinga hoja ya kutenga maeneo na nyadhifa katika uchaguzi mkuu ujao.

Wakizungumza mjini Mombasa, viongozi hao wamesema watahakikisha vyama vyao na ODM vinashindana katika nyadhifa zote za pwani, wakipuuzilia mbali madai kuwa ODM kinaungwa mkono zaidi katika eneo hilo.

Aidha, viongozi hao akiwemo Spika wa Seneti Amason Kingi na katibu wa chama cha UDA Hassan Omar wamesema ODM haipaswi kuweka masharti kwa Rais William Ruto, wakisisitiza kuwa ushirikiano wa sasa unalenga kuhakikisha anapata muhula wa pili.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *