#Athletics #Sports

OMANYALA ALENGA KUENDELEZA MAKALI ADDIS ABABA

Mwanariadha wa mbio fupi na mwenye kasi zaidi barani Afrika Ferdinand Omanyala anatarajiwa kuendeleza mwanzo wake mzuri wa msimu atakaposhiriki mashindano ya Grand Prix jijini Addis Ababa mwishoni mwa wiki hii.

Nyota huyo wa Kenya tayari alionyesha makali yake mapema msimu huu aliposhinda mbio za mita 100 katika mashindano ya Cape Milers yaliyofanyika Stellenbosch, Afrika Kusini, akitumia muda wa sekunde 10.19.

Sasa macho yote yataelekezwa Addis Ababa Jumapili, ambapo Omanyala analenga kuendeleza ushindi huo na kuthibitisha ubabe wake mapema katika msimu huu.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *