#Sports #Volleyball

KENYA PIPELINE YALENGA KUFUZU HATUA YA MTOANO, KCB YAANZA KAMPENI CAIRO

Timu ya mpira wa wavu ya  Kenya Pipeline inatarajiwa kufuzu hatua ya mtoano iwapo itapata ushindi wa tatu mfululizo katika mechi za awali za mashindano ya vilabu bingwa Afrika kwa wanawake.

Pipeline, inayowania taji la bara kwa mara ya kwanza baada ya miaka 20, itashuka dimbani saa kumi na mbili jioni kumenyana na timu ya La Loi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika kundi B.

Ushindi katika mechi hiyo utaifanya timu hiyo kufuzu hatua inayofuata baada ya ushindi wa seti za moja kwa moja dhidi ya Kalibi kutoka Ghana na Gender Light kutoka Burundi katika mechi zilizopita.

Wakati huo huo, mabingwa wa mwaka 2022 KCB Volleyball Club wataanza kampeni yao katika kundi D kwa kumenyana na timu ya Vipers kutoka Nigeria kuanzia saa kumi na moja jioni mjini Cairo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *