ERIC OUMA KARIBU KUREJEA UWANJANI
Mchezaji wa Harambee Stars, Eric Ouma maarufu kama ‘Marcelo’, yuko karibu kurejea uwanjani baada ya miezi tisa, akiwa na klabu yake ya Raków Częstochowa nchini Poland.
Mlinzi huyo wa kushoto mwenye umri wa miaka 29 alipata jeraha la kupasuka kwa kano la kisigino wakati wa mazoezi Agosti 28, 2025, jambo lililomwathiri pakubwa katika msimu wa 2025/2026 kwa klabu na taifa. Tangu wakati huo amekuwa akiendelea na mazoezi ya kupona jijini Nairobi kabla ya kurejea kwa klabu yake kufanyiwa uchunguzi zaidi.
Mchezaji huyo wa zamani wa Gor Mahia ameichezea Raków michezo 47 tangu ajiunge nayo mwaka 2024 akitokea klabu ya AIK ya Sweden, ambapo amefunga bao moja na kutoa pasi sita za mabao.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































