MARAGA AIKOSOA SERIKALI KUHUSU GHARAMA YA MAFUTA
Aliyekuwa Jaji Mkuu David Maraga ameikosoa serikali kwa kushindwa kuchukua hatua madhubuti za kuwalinda Wakenya dhidi ya ongezeko la gharama ya mafuta.
Akizungumza katika kaunti ya Nandi, Maraga amesema kupanda kwa bei ya mafuta kumesababisha gharama ya maisha kuongezeka kwa kiwango kikubwa, hali inayowafanya wananchi wengi kuishi kwa shida.
Ameongeza kuwa licha ya changamoto hizo, serikali inaendelea kutenga fedha nyingi kwa Ofisi ya Rais badala ya kuangazia mahitaji ya msingi ya wananchi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































