LUSAKA AWAFUTA KAZI MAWAZIRI WOTE
Gavana wa Bungoma Ken Lusaka anatarajiwa kuwateua mawaziri washikilizi kuhudumu kwenye baraza lake, baada ya kuvunjilia mbali baraza hilo hapo jana ambapo mawaziri wote, mwanasheria na katibu wa kaunti walifutwa kazi.
Kwa mujibu wa taarifa ya Lusaka, hatua hiyo inalenga kuimarisha utendakazi wa serikali yake na kuboreshwa kwa utoaji huduma kwa wakazi wa kaunti hiyo.
Amewahakikishia wakazi kuwa huduma hazitatizika kutokana na hatua ya kuvunjilia mbali baraza lake.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































