ZARIKA AWEKA MBELE LENGO LA MARUDIANO NA KIRSTY HILL
Bondia mkongwe wa Kenya Fatuma Zarika ameelekeza macho yake katika kutafuta pambano la marudiano na Kirsty Hill huku akiingia katika hatua ya mwisho ya taaluma yake ya ngumi.
Bondia huyo mwenye umri wa miaka 41 anatafuta nafasi nyingine ya kupigania taji la Ndondi la Jumuiya ya Madola katika uzani wa Super Featherweight, ambalo alipoteza kwa Hill kwa uamuzi wa majaji uliogawanyika mnamo Mei 2024 mjini Blackpool.
Licha ya kipigo hicho, Zarika ameendelea kushiriki mapambano, na tarehe 3 Aprili aliibuka na ushindi baada ya kumtwanga Flora Machela wa Tanzania katika raundi ya nane kwenye tukio la ngumi la SportPesa lililofanyika jijini Nairobi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































