#Sports #uncategorized

PAMZO AWARAI WAKENYA KUJITOKEZA KWA WINGI

BEKI wa zamani wa Harambee Stars, Sammy ‘Pamzo’ Omollo, amewataka Wakenya kujitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Kasarani wakati wa michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) ambayo inatarajiwa kuandaliwa kwa pamoja na Kenya, Uganda na Tanzania kuanzia wiki ijayo.

Kocha huyo mkuu wa Posta Rangers alitoa wito kwa Wakenya kuunga mkono timu yao ya taifa kwa hisia za uzalendo, huku akitoa imani kuwa Harambee Stars ilipewa nafasi ya kuweka historia kwa kunyanyua taji la CHAN katika mara yao ya kwanza ya kuomba.

Mtaalamu huyo mwenye umri wa miaka 55 pia alimtetea kocha wa timu ya taifa Bennie McCarthy, akimtaka kupuuza kelele za nje na kuangazia Kenya mapema Agosti 2. zikipangwa pamoja na Morocco, Angola, DR Congo, na Zambia huku mechi zote za Kundi ‘A’ zikitarajiwa kuchezwa jijini Nairobi.

Harambee Stars itacheza kwa mara ya kwanza michuano hiyo ambayo imetengewa wachezaji wa ndani, dhidi ya DR Congo mnamo Agosti 3 uwanjani Kasarani.Pumzo alisikitikia ugumu wa wawakilishi wa Kenya katika kandanda ya bara akisema umewaacha wachezaji wa ndani kukosa uzoefu wanaohitajika katika kiwango cha CHAN.

Imetayarishwa na Nelson Andati

PAMZO AWARAI WAKENYA KUJITOKEZA KWA WINGI

NA BADO, DPP INGONGA ASEMA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *