MIAKA 15 YA KATIBA YAADHIMISHWA
Sherehe za Siku ya Katiba zinaadhimishwa kwa mara ya kwanza hii leo ili kuadhimisha miaka 15 ya kuwepo kwa katiba mpya iliyopitishwa mwaka wa 2010.
Hafla hiyo itatumiwa kuangazia mafanikio chini ya katiba hiyo mbali na changamoto ikiwa ni miaka 15 ya utekelezaji wa katiba hiyo.
Sherehe hizo zitakuwa zikiadhimishwa kila tarehe 27 Agosti baada ya kutangazwa rasmi na Rais William Ruto mnamo Jumatatu wiki hii.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































