EPL: MAN UNITED KUVAANA NA WESTHAM
Ligi kuu ya uingereze inaendelea usiku wa leo mechi kadhaa zikiratibiwa kuchezwa. Mwendo wa saa nne unusu usiku kutakuwa na mechi tatu ambapo Tottenham Hotspur watakuwa wanaazimia kuweka masaibu ya wikendi kando watakapowaalika Newcastle huku kukiwa na presha kubwa kwa makocha wa timu hizo mbili. Mechi nyingine itakua kati ya Chelsea na Leeds katika uwanja wa Stamford Bridge wakati Everton wakikipiga dhidi ya Bournemouth. Baadaye mwendo wa saa tano na robo Manchester United watakuwa wakiangazia kuendeleza msururu wa matokeo mazuri watakapokuwa ugenini dhidi ya WestHam United.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































