#Local News

OTIENDE AONYA KUHUSU MGAWANYIKO NDANI YA ODM

Mbunge wa Rarieda, Otiende Amollo, ameonya kuhusu kuongezeka kwa mgawanyiko ndani ya chama cha Orange Democratic Movement, akisema mvutano huo unaweza kuathiri mazungumzo ya kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2027.

Akizungumza katika eneo bunge lake, Otiende amesisitiza kuwa anaendelea kuwa mwaminifu kwa chama hicho, lakini akakiri kuwa kimegawanyika katika makundi yanayopingana.

Aidha, Otiende ameonya kuwa migawanyiko hiyo inaweza kudhoofisha nguvu ya chama katika mazungumzo, akihimiza wanachama kukumbatia mazungumzo badala ya makabiliano.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

OTIENDE AONYA KUHUSU MGAWANYIKO NDANI YA ODM

WAMALWA AZUNGUMZIA VIFO KITENGELA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *