FAMILIA, WANAHARAKATI WASHINIKIZA HAKI KITENGELA
Wanaharakati na familia ya Vincent Ayomo, mwanamme aliyeuawa Jumapili iliyopita katika eneo la Kitengela kwenye mkutano ulioongozwa na katibu mkuu wa ODM Edwin Sifuna, wameshinikiza uchunguzi wa kina kufanywa ili wapate haki.
Ikiongozwa na mjane wake Winnie Ayomo, familia hiyo imesisitiza kuwa jamaa yao aliuawa na polisi waliiokuwa wakiutawanya umati, huku wanaharakati wakimtaka Waziri wa usalama wa kitaifa Kipchumba Murkomen na Inspekta Mkuu wa Polisi Douglas Kanja kujiuzulu kwa madai ya kushindwa kuwalinda wakenya.
Mamlaka ya IPOA imesema inachunguza matukio hayo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































