IEBC YAWAHIMIZA VIJANA KUJISAJILI
Tume huru ya uchaguzi na mipaka, IEBC, imewahimiza vijana kujisajili kwa wingi kama wapiga kura, kwa misingi kwamba malalamishi yao ya uongozi yanaweza tu kutatuliwa kwa kuwachagua viongozi walio na uwezo wa kuiendesha nchi.
Akizungumza kwenye kaunti ya Machakos, kamishna wa tume hiyo Alutalala Mukhwana, amesisitiza kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka ujao utawapa jukwaa zuri la kupaaza sauti yao.
Hata hivyo, amesisitiza kuwa mfumo wa uchaguzi hautabadilishwa kwa sasa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































