UPASUAJI WA MAITI WAFICHUA KIINI CHA KIFO MUKUMU
Imebainika kuwa mama mjamzito aliyefariki alipokuwa akijifungua katika hospitali ya kimisheni ya Mukumu kaunti ya Kakamega alifariki kutokana na majeraha na kuvunjika kwa viungo, familia ikishinikiza haki kutoka kwa hospitali hiyo.
Kwa mujibu wa ripoti ya upasuaji, mwathiriwa kwa jina Grace Wambui Misiko, alivunjika viungo vya mwili zikiwemo mbavu na sehemu ya uzazi.
Familia imesema wauguzi wa hospitali hiyo walimdhulumu hadi akafariki.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































