KOCHA WA LUANDA VILLA AAMINI TIMU ITANUSURIKA NSL
Kocha mkuu wa Luanda Villa, Francis Chinjili, amesema ana imani kuwa timu yake itaendelea kusalia katika Ligi ya Daraja la Kwanza, maarufu kama National Super League.
Chinjili amepuuza madai kuwa yuko chini ya shinikizo la kubadilisha hali ya timu hiyo ambayo imekuwa ikikumbwa na mabadiliko ya mara kwa mara ya makocha.
Tangu achukue usukani Januari 17mwaka huu, Chinjili ameiongoza timu hiyo kupata sare moja na kupoteza mechi nne, ikiwemo kichapo cha bao 1-0 nyumbani dhidi ya FC Talanta Jumapili iliyopita.
Hata hivyo, kocha huyo amesisitiza kuwa bado kuna nafasi ya kurekebisha makosa na kuhakikisha timu inasalia katika ligi hiyo msimu huu.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































