#Local News

IEBC YAONGEZA MATAYARISHO YA UCHAGUZI

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC imeimarisha matayarisho ya Uchaguzi Mkuu wa 2027 kupitia kongamano la washikadau kuhusu usajili unaoendelea wa wapigakura lililofanyika Kiambu.

Kongamano hilo limewaleta pamoja wadau mbalimbali kujadili mbinu bora za kuongeza idadi ya wapigakura wanaojiandikisha na kuboresha mchakato wa usajili nchini.

Tume hiyo imesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wadau wote ili kuhakikisha uchaguzi wa 2027 unafanyika kwa uwazi, ufanisi na ushiriki mpana wa wananchi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

IEBC YAONGEZA MATAYARISHO YA UCHAGUZI

TUJU AACHILIWA KWA DHAMANA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *