#Football #Sports

GOR MAHIA WATULIA KWENYE MBIO ZA UBINGWA

Mbio za ubingwa wa Ligi Kuu nchini zimepamba moto huku mabingwa watetezi Gor Mahia wakisalia watulivu licha ya presha kutoka kwa wapinzani wao wakuu AFC Leopards.

AFC Leopards wamepunguza pengo la alama hadi mbili baada ya ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya Murang’a Seal, huku Gor Mahia wakiongoza jedwali kwa alama 57 na wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

Kocha wao Charles Akonnor amesema hakuna hofu kambini, akisisitiza kuwa ubingwa uko mikononi mwao huku wakijipanga kwa mchezo muhimu dhidi ya Tusker wakilenga kutwaa taji lao la ishirini na mbili.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *