#Local News

WITO KWA VIJANA KUJISAJILI NYUMBANI

Huku zoezi la kuwasajili wapigakura wapya likiendelea kote nchini, vijana wametakiwa kujisajili kwa wingi katika maeneo wanakotoka.

Wito huo umetolewa huku kukiwa na madai kuwa baadhi ya viongozi wanawashawishi vijana kutoka sehemu nyingine kwenda kujisajili katika maeneo yao.

Wahusika wamesisitiza umuhimu wa uwazi na uadilifu katika zoezi hilo ili kuhakikisha haki na usawa vinazingatiwa katika mchakato wa uchaguzi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *