OCHUOGA AITAKA GOR MAHIA KUONGEZA UMAKINI
Beki wa klabu ya Gor Mahia, Paul Ochuoga, amewataka wachezaji wenzake kudumisha umakini na kasi kadri mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Kenya zinavyoingia hatua ya mwisho ya maamuzi.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka ishirini na moja amesema uthabiti na mtazamo chanya vitakuwa muhimu huku timu hiyo ikijiandaa kwa ratiba ngumu ya mechi dhidi ya Tusker , Kakamega Homeboyz, Bandari na wapinzani wao wa jadi AFC Leopards.
Gor Mahia wanaongoza msimamo wa ligi, lakini Ochuoga amesisitiza kuwa hakuna nafasi ya kuruhusu upole, akisema ubingwa unahitaji kumaliza kazi kwa nidhamu na umakini wa hali ya juu.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































