#Football #Sports

BANDARI YALENGA UBINGWA WA KOMBE LA FKF

Kocha wa makipa wa Bandari Razak Siwa, ameihimiza timu yake kuongeza bidii wanapolenga kutwaa Kombe la Shirikisho la Soka nchini na kujipatia nafasi ya kushiriki mashindano ya vilabu barani Afrika msimu ujao.

Siwa amesema wana uwezo wa kurudia mafanikio ya mwaka 2015 walipotwaa kombe hilo, akiongeza kuwa chini ya kocha mkuu Bernard Mwalala, timu hiyo ina nafasi nzuri ya kufanya vyema.

Kauli yake imekuja baada ya Bandari F kufuzu kwa robo fainali ya mashindano hayo kufuatia ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya timu ya daraja la pili ya 3K FC, mabao yaliyofungwa na Clifford Otieno na Joseph Otieno.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *