#Local News

UPINZANI WADAI VURUGU ZINACHOCHEWA NA SERIKALI

Huku mjadala kuhusu makundi ya wahuni kuzua vurugu katika mikutano ya kisiasa ukishika kasi, muungano wa upinzani nchini umeibua madai kwamba wahuni hao wanafadhiliwa na serikali kuvuruga mikutano ya upinzani.

Wakiwa katika hafla tofauti, kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka na mwenzake wa DCP Rigathi Gachagua, wamehofia kuwa huenda hatua ya serikali kushindwa kuyadhibiti makundi hayo ikasababisha kuibuka kwa makundi zaidi ya wahuni kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

Wameapa kuendeleza mikutano yao na wananchi.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *