BELLINGHAM ASEMA MECHI NA BAYERN ITAAMUA MSIMU WA REAL MADRID
Kiungo wa kati wa Real Madrid, Jude Bellingham, amesema mechi ya marudiano ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Bayern Munich ndiyo itakayoamua mustakabali wa msimu wa klabu hiyo.
Real Madrid wanakabiliwa na changamoto baada ya kupoteza mechi ya kwanza kwa mabao 2-1 dhidi ya Bayern Munich, ambao sasa wanahitaji angalau sare ili kufuzu nusu fainali.
Akizungumza mjini Munich, Bellingham alisema msimu wa Real unaweza kumalizika bila mataji iwapo watashindwa kusonga mbele katika mashindano hayo ya Ulaya.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































