#Local News

HUZUNI YATANDA KANDUYI BAADA YA MHUDUMU WA HOTELI KUUAWA

Hali ya huzuni imetanda katika soko la Tuuti Kibabii katika eneobunge la Kanduyi, baada ya mhudumu mmoja wa hoteli kupatikana akiwa ameuawa.

Kulingana na mmiliki wa hoteli hiyo, Yusufu Majaliwa, mfanyakazi wake alionekana kupitia kamera za usalama akianguka chini, jambo linalozua shaka kuwa alivamiwa usiku.

Wakazi na wafanyabiashara wa eneo hilo wamelalamikia kudorora kwa usalama, wakisema matukio ya uvamizi yamekuwa yakijirudia na sasa wanaiomba serikali kuingilia kati na kuimarisha ulinzi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *