SHUJAA WATARAJIWA KUNG’ARA HONG KONG
Timu ya taifa ya raga ya wachezaji saba Shujaa inaelekea katika mashindano ya Hong Kong Sevens ikiwa na matumaini mapya na kasi nzuri, huku ikisaka kurejea katika kiwango cha juu cha mashindano ya dunia.
Kocha wa Chuo Kikuu cha Kibabii, Peter Wamoto, ameonyesha imani kubwa kwa Shujaa, akisema wana uwezo wa kung’ara katika mashindano hayo kutokana na kiwango kizuri walichoonyesha hivi karibuni.
Wamoto amesema uthabiti wa timu hiyo katika mashindano ya karibuni umeifanya kuwa tishio kwa wapinzani na ina uwezo wa kufanya vyema katika jukwaa la kimataifa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































