#Football #Sports

KANE ASHANGAZWA NA KIWANGO CHA LUIS DIAZ

Mshambuliaji wa Bayern Munich Harry Kane amemsifu Luis Díaz kwa bao la dakika za mwisho alilolifunga na kuipa timu yao ushindi muhimu dhidi ya Real Madrid katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Bayern walikuwa na faida ya mabao 2-1 kutoka mechi ya kwanza, lakini walijikuta wakiruhusu mabao kadhaa katika mchezo wa marudiano huku Real Madrid wakionyesha kiwango cha juu walichozoea katika mashindano ya Ulaya.

Jumla ya mabao ilikuwa sare ya 4-4 hadi dakika ya 89 ambapo Díaz alipata bao la ushindi, kabla ya Michael Olise kuongeza bao lingine dakika za nyongeza na kuithibitishia Bayern Munich nafasi ya kutinga nusu fainali.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *