#Rugby

KAKAMEGA HIGH WAJIPANGA KWA MASHINDANO YA RAGA YA WACHEZAJI SABA

Kocha mkuu wa raga wa shule ya Kakamega High Amos Wamanga amesema timu hiyo sasa imehamisha mwelekeo wake kuelekea mashindano ya wachezaji saba baada ya kumaliza katika nafasi ya nne kwenye mashindano ya kitaifa ya wachezaji kumi na watano

Wamanga amesema timu ilijitahidi kadri ya uwezo wao katika mashindano hayo na kueleza kuridhishwa na kujituma kwa wachezaji huku akiongeza kuwa ana imani kikosi hicho kina uwezo wa kushinda taji la kitaifa la wachezaji saba

Amebainisha kuwa kuitwa kwao kushiriki mashindano hayo kwa dharura baada ya kuchukua nafasi ya Bungoma High kulifanya washindwe kuandaa kikosi kilicho katika hali bora kabisa lakini anaamini watafanya vyema katika hatua inayofuata.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *