MUKHISA AAGIZWA NA CUE KUHUSU MADAI DHIDI CHUO
Tume inayosimamia elimu ya vyuo vikuu, CUE, imemwagiza aliyekuwa katibu mkuu wa idara ya biashara na ustawi chini ya Umoja wa Mataifa, Mukhisa Kituyi, kufika mbele yake kuhusiana na kauli alizotoa kuhusu chuo kikuu cha Masinde Muliro.
Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, CUE imesema Mukhisa, akiwa kwenye mahojiano na kituo cha redio tarehe 31 mwezi jana, alidai kwamba kuna watu waliopewa nafasi na chuo hicho kufuzu ila hakuwa wanafunzi wa chuoni humo.
Tume hiyo imemtaka ajiwasilishe na ushahidi kuhusu madai yake.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































