#Football #Sports

EPL: MAN U KUTOANA KIJASHO NA CHELSEA, ARSENAL KUKAZA NATI DHIDI YA MAN CITY

Ligi kuu ya uingereza inarejea wikendi hii kwa kishindo huku mbio za ubingwa zitazamiwa kuamuliwa. Hapo kesho Brentford watakua mbioni kusaka nafasi za ulaya wakiwakaribisha Fulham, Leeds wavaane na Wolves, Newcastle wakaribishe Bournemouth huku Tottenham wakipambana kujikwamua dhidi ya kushushwa daraja watakapomenyana na Brighton. Saa nne mechi kali ya siku itawahusisha Chelsea wakiwa Stamford Bridge watakapokaribisha Manchester United. Siku ya Jumapili Aston Villa watakaribisha Sunderland wakati Everton wakiwa nyumbani dhid ya Liverpool kwenye Merseyside derby. Saa kumi na mbili Unusu Mbio za ubingwa zitaamuliwa wakati Manchester City watakapokua nyumbani kupambana na Arsenal.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *