YIEMBE AITWA KUCHEZESHA KOMBE LA DUNIA LA KLABU 2025
Msaidizi wa refa wa FIFA, Stephen Yiembe, atahudumu kandokando ya uwanja kwenye michuano ya Kombe la Dunia la Klabu la FIFA 2025, akiungana na kundi la maafisa wa mechi 117 walioteuliwa na shirikisho hilo la soka duniani kwa ajili ya mashindano hayo yatakayofanyika kuanzia tarehe 14 Juni hadi 13 Julai 2025 nchini Marekani.
Yiembe ni mwakilishi pekee kutoka Afrika Mashariki aliyechaguliwa na ana tajriba kutoka mechi za kimataifa, ikiwemo ile kati ya Senegal na Togo, Pia amejumuishwa kwenye waamuzi wa Olimpiki ya Paris 2024.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































