OLUOCH AOMBOLEZA PAUL OTULA
Kocha mkuu wa mpira wa vikapu wa timu ya Chuo Kikuu cha Africa Nazarene Michael Oluoch amemuomboleza marehemu rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu nchini Paul Otula, akimtaja kama nguzo katika chama cha mpira wa vikapu nchini.
Oluoch anasema kufariki kwa Otula sio tu pigo kwa udugu wa mpira wa vikapu bali kwa taasisi ya mafunzo ya mchezo huo.
Otula, ambaye aliaga dunia Alhamisi iliyopita baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo nyumbani kwake Nairobi, pia aliwahi kuwa mwalimu Mkuu wa Shule ya upili ya Maseno.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































