SHA YAINGIA GEREZANI
Serikali imeimarisha juhudi zake za kuhakikisha kila mkenya anasajiliwa chini ya bima ya afya ya kitaifa SHA, sasa ikianzisha zoezi la kuwasajili wafungwa katika magereza yote nchini.
Zoezi hilo linajumuisha utoaji wa vitambulisho kwa wafungwa, limezinduliwa katika gereza la wanawake la Lang’ata, likiongozwa na makatibu Ouma Oluga wa afya, Belio Kipsang wa uhamiaji, Salome Beacco wa magereza na Chepkirui Rono wa masuala ya bunge.
Kwa mujibu wa serikali, zoezi hilo ni mojawapo ya miakakti ya kuhakikisha afya ya wote UHC inafikiwa na kila mkenya.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































