BASTOLA ILIYOTUMIKA KUMWUA MBUNGE WERE YANASWA
Uchunguzi katika kuwanasa waliohusika na mauaji ya aliyekuwa mbunge wa Kasipul Ong’ondo Were umepiga hatua kubwa, polisi wakitangaza kupata bunduki iliyotumika kutekeleza mauaji hayo ya wiki jana.
Akiwahutubia wanahabari, Inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja amesema uchunguzi kuhusu matumizi ya bunduki umebainisha kwamba bastola iliyonaswa kutoka kwa mmoja wa washukiwa ndiyo iliyotumika.
Ameongeza kuwa bastola hiyo pia imehusishwa na visa vingine vitatu vya ujambazi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































