ONG’ONDO: MAWAKILI WADAI DHULUMA DHIDI YA MSHUKIWA
Mawakili wa mfanyabiashara Philip Aroko anayezuiliwa katika kituo cha polisi cha Gigiri kwa kuhusishwa na mauaji ya mbunge Ong’ondo Were, wameibua hofu ya haki za mteja wao kukiukwa, wakisema amezuiliwa bila mashtaka huku wakimzuia kukutana na mawakili, familia na marafiki zake.
Katika hatikiapo ambayo imewasilishwa kwenye mahakama kuu, mawakili wakiongozwa na Danstan Omari wamesema juhudi zao za kutaka aachiwe huru kwa dhamana ya polisi zimekosa kufaulu.
Wameitaka mahakama kuingilia kati, wakihofia kwamba huenda mteja wao akazuiliwa kwa muda mrefu kinyume na katiba.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































