#Business

KPA KUONGEZA UWEZO WA BANDARI KWA TANI MILIONI 47

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini KPA inaendeleza mpango wa upanuzi na uboreshaji wa mabilioni ya dola ili kukidhi mzigo unaotarajiwa wa tani milioni 47 za shehena ndani ya miaka mitano. Mnamo mwaka wa 2024, KPA ilihudumia tani milioni 41.1, ikiwa ni ongezeko la asilimia 14.1% kutoka tani milioni 36.0 mwaka wa 2023.

Muhimu katika mpango huo ni ujenzi wa Awamu ya Tatu ya Kituo cha Pili cha Kontena, ambacho kitaongeza uwezo kwa TEU 500,000, kulingana na ripoti ya Standard. Ukaguzi umeidhinisha upanuzi huo utakaofanywa kwa ushirikiano kati ya KPA na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Japani (JICA).

Ingawa gharama kamili ya awamu ya tatu bado haijafichuliwa, Awamu ya Kwanza iligharimu Ksh26 bilioni, na Awamu ya Pili—yenye gati tatu—ilikuwa na thamani ya takriban Ksh32 bilioni.

Imetayarishwa na Mercy Asami

KPA KUONGEZA UWEZO WA BANDARI KWA TANI MILIONI 47

HATUA KUBWA YA AFYA MAKUENI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *