BABU ATETEA KILIMO, UJENZI
Mbunge wa Embakasi East Babu Owino ameionya kamati ya fedha katika bunge la kitaifa dhidi ya kuongeza ushuru kwenye mswada wa kifedha wa mwaka 2025-26, akisema hatua hiyo italemaza sekta ya kilimo na uchumi kwa jumla.
Akizungumza mbele ya kamati hiyo inayoongozwa na mbunge wa Molo Kimani Kuria, Owino ametaja sekta za kilimo, ujenzi na uzalishaji kuwa nguzo za uchumi, na jaribio la kuongeza ushuru kwenye sekta hizo zitaathiri uchumi wa taifa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































