#Local News

MIGOSI ATAKIWA KUWEKA WAZI MIRADI YA ELIMU

Wizara ya elimu imetakiwa kuorodhesha miradi yote inayoendeshwa katika shule zilizoko maeneo bunge tofauti nchini na ripoti hiyo kuwasilishwa mbele ya kamati ya bunge kuhusu elimu.

Waziri wa elimu Julius Migosi akiwa mbele ya kamati ya bunge ametakiwa kuwashirikisha wabunge na wakuu wengine wa elimu katika ujenzi wa miradi katika shule zilizoko katika maeneo bunge yao ili kusaidia katika kufanikisha ukamilishaji wa miradi hiyo.

Haya yanajiri huku wizara hiyo ikidai kukosa fedha za kutosha kuendesha shughuli zake.

Imetayarishwa na Maureen Makhobe

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *