AFCON YAKABILIWA NA MKANGANYIKO
Maandalizi ya Kenya kwa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 yamekabiliwa na mkanganyiko mkubwa baada ya ufinyu wa bajeti kwa idara ya michezo, huku kukiwa na kupunguzwa kwa ufadhili katika idara hiyo.
Makadirio ya bajeti yaliyopendekezwa kwa mwaka wa kifedha wa 2025-2026 yaliyowasilishwa bungeni wiki hii, yanaonyesha kupunguzwa kwa Ksh.1.1 bilioni kwa Idara ya Michezo.
Hili limezua sintofahamu juu ya mada ambayo tayari ina utata kuhusu utayari wa Kenya kuandaa hafla za kimataifa, huku ikiibua shaka juu ya uwezo wa Kenya wa kuwa mwenyeji.
Hii ina maana kwamba Ksh.3.9 bilioni zilizokuwa zimetengwa mahususi kama ada ya haki za uandaaji-shirikishi wa mashindano hayatolewi.
Kenya inatazamiwa kuwa mwenyeji mwenza wa makala ya 36 ya kilele cha soka ya kitaifa barani Afrika pamoja na majirani wa Uganda na Tanzania.
Mawaziri la Michezo Salim Mvurya, katika wasilisho lake la Mei 19, 2025, kwa Bunge la Kitaifa alieleza udharura wa kutenga fedha hizo kutimiza ahadi ya Kenya.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































