#Local News

OCS TAALAM KUJUA HATMA KESHO

OCS wa kituo cha polisi cha Central Samson Taalam ataendelea kukesha katika kituo cha polisi cha Lang’ata hadi hapo kesho ambapo mahakama itaamua ombi lake la kupewa dhamana kwenye kesi inayomkabili kuhusiana na mauaji ya bloga Albert Ojwang.

Kwenye kesi hiyo, mamlaka ya kutathmini mienendo ya maafisa wa polisi IPOA imeomba mahakama itoe amri ya kumzuilia Taalam kwa siku 21 zaidi ili kukamilisha uchunguzi dhidi yake, ikizingatiwa kuwa amehusishwa moja kwa moja na mauaji hayo.

Imetayrishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *